Shirika la Afya Duniani WHO limetoa tamko rasmi leo Jumanne la kusisitiza kwamba ugonjwa wa homa ya nyani unaosababishwa na virusi vya mpox, sio ugonjwa mpya wa UVIKO unaosababishwa na virusi vya corona.

Tamko hilo limetolewa baada ya kuibuka kwa aina mpya ya kirusi cha clade 1 kinachosambaa kwa kasi barani Afrika na ambacho kimezusha wasiwasi kimataifa.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya Hans Kluge amewaambia waandishi wa Habari kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kwamba inafaa kuishughulikia mpox kwa pamoja katika kuweka mifumo ili kuidhibiti na kuitokomeza kimataifa.

Msemaji wa shirika la afya duniani Tarik Jasarevic amesema WHO kwa sasa haijatoa mapendekezo ya watu kuvaa barakoa.

Please follow and like us:
Pin Share