Serikali ya Kenya imesema italazimika kurejesha baadhi ya hatua za ulipaji kodi ambazo zilifutwa baada ya kuibuka maandamano makubwa mwezi Juni.

Hatua ya Serikali ya Kenya ni jambo linalozidisha hatari ya kutokea machafuko zaidi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo John Mbadi aliyesisitiza kwamba baadhi ya hatua zitarekebishwa, lakini akasema zinahitajika ili kumudu matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara ya walimu.

Baada ya kauli hiyo ya Waziri Mbadi aliyoitoa jana usiku wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha CItizen, baadhi ya watu walioshiriki maandamano yaliyoongozwa na vuguvugu la vijana maarufu kama Gen-Z wamesema wako tayari kuingia tena mitaani na kuandamana.

Please follow and like us:
Pin Share