Ma Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

Makamu wa Rais , Dkt. Philip Isdori Mpango ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Ibihwa, Wilayani Bahi, Mkoani Dodoma,

Dkt. Mpango amesisitiza kuongeza kasi ya uchimbaji wa visima ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama, na ahadi ya kukamilisha mradi wa maji katika kijiji hicho ikamilike ifikapo tarehe Septemba 30, 2024.

Waziri wa Maji,  Jumaa Aweso amewahakikishia wananchi wa Kijiji cha Ibihwa kuwa, Wizara itakamilisha mradi huo kabla ya tarehe 30 Septemba, 2024 na huduma ya maji itafika katika mji wa Bahi.

Mradi wa Maji wa Ibihwa unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 709 na unasimamiwa na Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) huku  utekelezaji wake ukiwa umefika asilimia 75 na umeanza kutoa huduma kwa wananchi, na kutarajiwa kunufaisha wananchi zaidi ya 8000 wa Kijiji cha Ibihwa.

Please follow and like us:
Pin Share