JESHI la Israel limesema limemuua hivi leo kamanda wa kundi la wanamgambo la Hezbollah katika shambulio la anga kusini mwa Lebanon. Mwanamume huyo aliuawa karibu na mji wa pwani wa Tiro.

Awali, Wizara ya Afya ya Lebanon ilitangaza kwamba mtu mmoja aliuawa katika shambulizi la Israel lililolenga pikipiki katika eneo hilo.

Jeshi la Israellimesema aliyeuawa alikuwa kamanda wa kikosi cha Radwan, kitengo cha wasomi ndani ya kundi hilo la Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran. Kundi hilo halikutoa tamko lolote juu ya shambulizi hilo wala madai ya Israel.

Mara kwa mara, Hezbollah imekuwa ikirusha roketi kutoka kusini mwa Lebanon hadi kaskazini mwa Israel tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israel limejibu kwa mashambulizi mengi ya anga pamoja na mashambulizi ya makombora na kuyalenga maeneo ya kusini mwa Lebanon.

Please follow and like us:
Pin Share