Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Rais wa Jamhuri ya Botswana Mhe. Dkt. Mokgweetsi Masisi wakati viongozi kutoka mataifa mbalimbali wakiingia kwenye mkutano  wa 44 wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC unaofanyika Jengo jipya la Bunge la bunge la Zimbabwe (New Parliament Building) lililoko katika eneo la kilima cha Mount Hapdeo jijini Harare leo Agosti 17, 2024.

Rais wa Zimbabwe Mhe. Emerson Mnangagwa kushoto akiongozana na Rais wa Angola Mhe. Joao Lourenco wakielekea ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kushiriki mkutano huo unaofanyika Harare Zimbabwe. 

Kutoka kulia ni Rais wa Afrika Kusini Mhe. Ciril Ramaphosa, Mfalme Mswati wa Lethoto  na Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera wakiwasili katika ukumbi tayari kwa ajili ya kushiriki mkutano huo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Marais wa nchi wanachama wa  SADC  kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa 44 wa SADC jijin Harare Zimbabwe. 

Bendera za nchi wawanachama wa SADC zikipepea nje ya jengo la Bunge la Zimbabwe. 

Please follow and like us:
Pin Share