Na Stella Aron, JamhuriMedia, Zimbabwe

Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Sululu Hassan kwa usimamizi bora wa demokrasia na kuwa Tanzania ya mfano.

Akizungumza kwa njia ya mtandao wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC -Organ Troika Summit), mwenyekiti wa asasi hiyo Rais wa Zambia Hakainde Hichilema nchini Zimbabwe.

Rais Hakainde Hichilema wa Zambia akizungumza kwa njia ya Mtandao katika kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- Organ Troika Summit) jijini Harare Zimbabwe. 

Hichilema amesema Rais Dkt. Samia ameaminiwa kwa kusimamia uenyekiti wake hata kabla ya kukabidhiwa uongozi kama mwenyekiti ajaye.

“Tanzania imekuwa mfano bora hususani katika demokrasia pamoja na kuaminiwa na wakuu wa nchi wote wa nchi za SADC” amesema.

Mhe. Hichilema ameongeza kwamba yeye mweyewe anamuunga mkono na yuko tayari kumsaidia kwa nguvu zote wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ Troika Summit).

Mkutano wa wakuu wa nchi na viongozi wa Serikali wa SADC unaofanyika katika jengo jipya la Bunge la Zimbabwe (New Parliament Building) lililoko katika eneo la kilima cha Mount Hapdeo jijini Harare.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan atapokea uenyekiti wa asasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kutoka kwa Rais Hakainde Hichilema wa Zambia anayemaliza muda wake wa uongozi.

Please follow and like us:
Pin Share