Na Magrethy Katengu–Jamuhuri Media Dar es salaam

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kazi vijana ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi amesema Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea na programu ya kuwatambua makundi ya vijana ili kutengeza sera zinazojibu mahitaji yao ikiwemo kuwakwamua kiuchumi ili waweze kujiaji wenyewe pasipo kutegemea kuajiriwa.

Ameyasema hayo Agosti 15, 2024 ikiwa na maadhimisho ya siku ya vijana Duniani yakiambatana na Maadhimisho ya mwaka mmoja ya taasisi ya Amo faundation ambapo amebanisha kuwa mamlaka zinatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili vijana kwa kutunga sera zenye majibu ya vijana .

“Wajibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuhakikisha tunawatambua vijana waliosoma na wasiosama , walio na fursa na wasio na furasa, aliye na mtaji na asiye na mtaji, Yatima na asiye yatima ili kuwakwamu wote kiuchumi wasiwe na malalamiko kila leo kusema hakuna ajira wakati fursa zipo ikiwemo mikopo ” amesema Naibu Waziri

Naye Mkurugenzi wa taasisi ya Amo faundation Amina Saidy Good hii taasisi inashirikiana na Serikali ili kuwainua vijana kwa kuwapatia mitaji kupitia ujuzi walio nao wengine kupatiwa mikopo na hadi sasa wametimiza mwaka mmoja kuna vijana wengi wamenufaika kupitia Amo kwa kujikwamua kiuchumi badala ya kuwa tegemezi na kusubiria ajira ambazo zimekuwa chache.

Naye Geradi Musa amesema siku hiyo ni adhimu sana kwa vijana kutokana na ukosefu wa ajira uliopo hawana budi kutumia majukwaa kwa hayo kutambua fursa zilizopo kwani kwa sasa mitandao ya kijamii imekuwa chachu kubwa kwa baadhi ya vijana kuitumia kufanya biashara mtandao na kupata fedha

Aidha katika maadhimisho hayo ya vijana yaliyoambatana na mwaka mmoja wa Amo faundation Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan Zungu naye alihudhuria kuwafunda vijana namna ya kujikwamua kiuchumi kupitia fursa zilizopo nchini kupitia taasisi mbalimbali na serikali.

Please follow and like us:
Pin Share