Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) kukomesha wizi wa mita za maji ambao hivi sasa umekithiri katika maeneo mbalimbali jijini humo.

Chalamila ameyasema hayo alipokuwa katika ziara katika Jimbo la Kibamba ,ambapo alikagua miradi ya mbalimbali ikiwemo ya nyumba ya mkurugenzi , barabara na mradi wa maji ambao aliukataa kutokana na changamoto iliyokuwepo.

Chalamila amesema DAWASA wanatakiwa kujipanga upya kutekeleza miradi ya maji ,sambamba na kutokomeza wizi wa mita kama walivyofanya TANESCO kwani mpaka sasa kuna zaidi ya mita 900 zimeibiwa.

“Haiwezekani mita zifungwe alafu zibiwe ofisi ya mkuu wa mkoa na wilaya, mnatakiwa kujiunga na DAWASA kuweka mikakati madhubuti ya kutokomeza kabisa wizi huu kwa sababu Rais anawekeza pesa nyingi katika miradi ya maji nahitaji maelezo ya kina.

Siwezi kukubali kupitisha mradi huu ,kwa mwananchi mmoja nahitaji nione wananchi wengi wanasema wamenufaika na huduma lakini sio mtu mmoja pekee kama mlivyofanya leo japokuwa kuna busta imefungwa lakini bado kuna makelele mengi kwenye sekta ya maji eneo hili kwa jamii“amesema.

Amesema wezi wa mita wanaishi katika jamii hawajakwenda likizo, hivyo wanatakiwa kuzibitiwa haraka kabla ya hali kuwa mbaya zaidi.

Kwa upande mwingine Chalamira amewataka watanzania kudumisha amani ya nchi, kwa kufanya siasa za kistarabu kwa manufaa ya nchi.

Chalamila amesema wananchi na viongozi wasiogope kuwataja viongozi wenye mienendo mibovu na wala rushwa kwasababu ya kuogopa kufukuzwa kwasababu chama hakimpendi wenye tabia hizo.

Amesema wananchi wanatakiwa kuchagua viongozi walio sahihi wenye kumsadia Rais katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutangaza mazuri yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ,kwani yeye hawezi kufika kila eneo ni wajibu wao kutekeleza mandeleo yanayotolewa na Serikali katika maene yao.

Katika ziara hiyo Chalamila ameridhika na mradi wa nyumba ya mkurugenzi na barabara ,ambapo alimtaka mkandarasi kuendelea na kazi.

Mkuu wa wilaya ya Ubungo Hassani Bomboko amesema ukichana na changamoto hiyo bado DAWASA hawatendi haki kwa wananchi hasa katika kwenye usomaji wa mita na uandikaji bili .

Bomboko amedai amefanya ziara katika kata hiyo na kugundua kuna uwepo wa maji, katika baadhi ya maeneo ya Wananchi wanakaa zaidi ya miezi mitatu bila maji na mita zinasoma ametumia unit moja mbili alfu kwenye bili zinakuja kubwa kuliko matumizi

Kwa upande mwingine amesema bado kuna changamoto ya simamizi wa ujenzi wa barabara za ndani ,zinazo simamiwa na Mamlaka ya Barabara vijijini TARURA, Mkandarasi kakimbia city eneo Suka Golani waliposikia kiongozi anakwenda wakapeka vifaa vyao na pale anapoondoka na wao wanaondoka eneo hilo.

“Sasa leo nataka watueleze kama pesa zipo kinashindikana nini ,kwa sababu wanataka kutuchonganisha na wananchi wetu” amesema.

Amempongeza Rais Samia kwa kuwapatia bilioni 100 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo ambayo imefikia katika hatua nzuri hasa sekta ya afya ambayo kwa sasa huduma imeimarika.

Please follow and like us:
Pin Share