Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Arusha 08/08/2024 majira ya saa mbili usiku katika maeneo ya Kisongo imekamata raia (04) wa Ethiopia kwenye gari aina ya Toyota Land Cruser Station Wagon GX yenye namba za usajili T 801 AGJ, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema. Dereva wa gari hilo pamoja na watuhumiwa wengine walipobaini kuna mtego wa kuwakamata walikimbia na kutelekeza gari hilo pamoja na watuhumiwa hao 4 katika shamba la mahindi.

Aidha, Leo 09/08/2024 majira ya saa nne asubuhi maeneo ya Duka bovu, Maafisa Uhamiaji wa Wilaya ya Monduli wamefanikiwa kukamata raia (02) wa Ethiopia na (01) raia wa Somalia ambao walikuwa miungoni mwa watuhumiwa (4) waliokamatwa usiku wa 08.08.2024 hivyo kufanya idadi yao kuwa (7).

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji SACI Fakih Nyakunga akizungumza na vyombo vya habari Leo hii amethibitisha kukamatwa kwa raia hao (07), ambao (06).

Please follow and like us:
Pin Share