Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dodoma

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Islands of Peace Tanzania limesema kuwa mpaka sasa limeweza kuwafikia wakulima zaidi ya 3500 katika kuhamasisha na kughuhisha mifumo endelevu ya chakula kwa kutumia kilimo Ikolojia.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo, Asyesiga Buberwa mara baada ya kutembelewa na Balozi WA Marekani nchini Tanzania, Dkt. Michael Battle katika banda lao lililopo katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Amesema kuwa Shirika la Islands of Peace Tanzania linafanya kazi na wakulima wadogo wenye kumiliki ya ekari chini ya tatu waliopo vijijini ambao hata uwezo wa kununua pembejeo hawana.

“Sisi pia ni wanufaika na ufadhilinwa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), ambapo kazi yetu kubwa ni kuhamasisha na kughuhisha mifumo endelevu ya chakula kwa kutumia kilimo Ikolojia.

“Tumefurahishwa na kutembelewa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania pamoja na timu yake ambao wamekuja kuona wakulima wetu wanafanya nini kwenye suala zima la kutunza, kuhifadhi na kuendeleza mbegu zetu za asili,” amesema.

Aidha amesema wanaendelea kuwahawasisha wakulima hao na kwamba wanafanya kazi na Shirikisho la Vyama vya Wakulima Wadogo Tanzania ambalo linawafikia wakulima zaidi ya 45,000 nchini.

Amesema kuwa Balozi Dk.Battle na timu yake wameona ni jinsi gani vijana wanaweza kujikita katika masuala ya kilimo kwenye maeneo zaidi ya kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao, kutengeza mbolea za asili kwa kutumia mbinu mbalimbali ambazo ni bunifu zinazowaletea kipato.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wao kama Shirika la Islands of Peace Tanzania wanafurahi kuwa miongoni mwa watu wanaofadhiliwa na shirika la USAID, huku akiishukuru serikali ya Marekani kwa ufadhili wake.

Akizungumza mara kutembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa, Taasisi, Makampuni na Mashirika yanayofadhiliwa serikali ya Marekani USAID ambayo yameshiriki katika maonesho hayo, Balozi Battle amesema kuwa serikali ya Marekani inawekeza Mamilioni ya fedha za Kimarekani hapa nchini Tanzania na Marekani ndio mfadhili mkubwa wa shuguli za kimaendeleo.

Please follow and like us:
Pin Share