Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

Bodi ya Bima ya Amana(DIB)ikiwa na jukumu muhimu katika usimamizi na udhibiti wa sekta ya bima nchini imesema itaendelea kudhibiti , kusimamia na Kufuatilia kampuni zote za bima kuhakikisha zinazingatia sheria na kanuni ili kuweka viwango vya maadili na kuimarisha uwazi katika utendaji wa kampuni za bima.

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)na Mwenyekiti Wa bodi ya wakurugenzi Wa bodi ya bima ya Amana Emmanuel Jutuba ameeleza hayo leo Agosti 7,2024 kwenye maonesho ya wakulima yanayoendelea Nzuguni kwenye uwanja wa Nanenane Dodoma na kueleza kuwa majukumu ya bodi hiyo ni kukagua na kutoa leseni kwa kampuni za bima ili kuhakikisha zinafaa kuendesha shughuli za bima.

Ametaja majukumu mengine kuwa ni pamoja na kutathmini Malalamiko kwa kupokea na kuyatatua kutoka kwa wateja kuhusu huduma za bima.

“Natoa wito kwa wananchi kutembelea banda la Bodi ya bima ya amana kujifunza zaidi, wanapaswa kuelewa kuwa tunaendeleza na kuboresha mazingira ya biashara ya bima kwa ajili ya kukuza ukuaji wa sekta hii ili kuhakikisha sekta ya bima inafanya kazi kwa ufanisi na kwa faida ya wateja, “ameeleza.

Amesema, ” Sisi kama benki kuu tunaendelea kusimamia benki zisitetereke ambapo tupo katika mchakato wa kuboresha muundo wa kisheria na kiutendaji ili kuchangia kikamilifu na kwa kwa ubora na mchakato huu unalenga kuifanya Bodi ijitegemee kiutendaji, “amesisitiza Gavana huyo

Ameeleza ukubwa wa mfuko huo kuwa hadi kufikia June 30,2023 Mfuko wa bima ya amana ulikuwa na shilingi Trilioni 1.04 ambazo zimetokana na mchango wa Serikali wa shilingi Bilioni 1.05 ambazo zilitolewa wakati wa kuanzisha mfuko mwaka 1994 na kufafanua kuwa hadi kufikia June 30,2024 mfuko ulikuwa na wanachama 44.

Mbali na hayo ameeleza muundo wa Bodi hiyo kuwa upimo chini ya Mamlaka ya Bodi ya wakurugenzi ambayo ina jukumu la kuunda Sera na kuhakikisha utawala bora.

“Kwa mujibu wa Sheria iliyounda bodi ya bima ya amana, Bodi ya wakurugenzi ya bodi ya amana imejumuisha wajumbe wanaotoka BoT ambaye ni Gavana, Mwakilishi wa wizara ya fedha, Katibu Mkuu wizara ya fedha na Wajumbe wengine watatu wanaochaguliwa na Waziri wa fedha, “amesema

Ikumbukwe kuwa DIB ni Taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya benki na Taasisi za fedha ya mwaka 1991 ambapo ilianza kufanya kazi zake mwaka 1994 chini ya usimamizi wa BOT.

Please follow and like us:
Pin Share