Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

KAMANDA wa Takukuru Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda amepongeza wakala wa bara bara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoani humo kwa kufanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika kipindi cha mwaka fedha 2022/2023 bila uwepo wa changamoto kwenye miradi hiyo iliyotekelezwa.

Mwenda amezitoa pongezi hizo leo wakati wa Hafla fupi ya utiaji saini mikataba ya matengenezo ya barabara za vijijini na mjini kati ya Tarula na wakandalasi mkoani Ruvuma kwa mwaka wa fedha 2024/2025 iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Nkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa Mkoa wa mkoa huo Kanali Ahamed Abbas Ahamed.

Alisema kuwa mikataba iliyosainiwa jana itakwenda kufanya kazi kwa viwango vinavyokubalika kwa kila mpenda maendeleo wa Mkoa wa Ruvuma ambapo katika kipindi cha mwaka jana wakala wa barabara mijini na Vijijini (Tarula) walifanya kazi nzuri japokuwa kulikuwa na kasoro ndogo ndogo ambazo nazo tayari zilishafanyiwa kazi hivyo wakandarasi walioingia mikataba ya kutengeneza miundombinu ya barabara katika kipindi cha mwaka 2024/2025 wanapaswa kufanya kazi kwa weledi mkubwa na si vinginevyo.

‘’Nichukuwe fursa hii kuwaarifu wenzetu wakandarasi pamoja na watumishi wa Tarula kwamba sisi kama taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) tunamaelekezo mahususi toka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhuu Hassan ya kufuatilia utekelezaji wa miradi hii ya barabara na kuhakikisha kwamba inafanyika kwa viwango vinavyotakiwa.’’alisema Mwenda.

Hata hivyo Mwenda amewataka wakala wa barabara mjini na vijijini (Tarula) kuona umuhimu wa kusimamia kikamilifu miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara kabla ya kuwalipa fedha wakandarasi wanapaswa waende kwenye maeneo ya miradi ndipo malipo yafanyike ili kuepuka malipo hewa yanayoweza kusababishwa kufikishwa mahakamani.

Kwa upande wake meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijijini(Tarula) mkoani Ruvuma Mhandisi Silvester Chinengo alisema kuwa mwaka wa fedha 2024/2025 wameidhinishiwa kiasi cha fedha sh. Bilioni 22 kwaajiri ya matengenezo ya barabara na madaraja kwenye mtandao wao ambapo katika kiasi hicho cha fedha kiasi cha sh. Bilioni 7.89 zinatoka kwenye mfuko wa barabara, sh. Bilioni 4.5 zinatoka mfuko mkuu wa serikali kwa maana ya mfuko wa majimbo na sh. Bilioni 9.79 zinatoka kwenye tozo ya mafuta.

Meneja wa TARURA MKOA WA Ruvuma mhandisi Silvester Chinengo akikabidhi moja ya kitabu kwa wakandarasi.

Alisema kuwa bajeti hiyo itaenda kufanya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 1,145.73 itajenga madaraja 50 na makaravati 57 ambapo mpaka sasa Tarula imekamilisha mikataba ya manunuzi 50 ambayo ni ya awamu ya kwanza yenye gharama ya fedha za kitanzania kiasi cha sh. Bilioni 14.7.

Nae mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abass Ahamed katika afla hiyo ya utiaji wa saini ya mikataba kwaajiri ya ujenzi wa miundombinu ya barabara alisema kuwa ni hatua kubwa kwa maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma kuwa na matarajio makubwa kwaajiri ya matengenezo mbalimbali ya barabara ,madaraja na makalavati kwani uchumi wa nchi unategemea sana miundombinu ya barabara.

‘’kama nilivyosema tumekutana hapa kwaajiri ya tukio muhimu la mkoa wa Ruvuma ambapo taarifa ya uongozi wa wakala wa barabara Mjini na vijijini (Tarula) mkoa wa Ruvuma umesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 katika bajeti ya miundo mbinu ya barabara umeidhinishiwa jumla y ash. Bilioni 22.1 ambazo zitakwenda kutengeneza miundombinu ya barabara katika Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ‘’alisema Kanali Ahamed

Alieleza Zaidi kuwa wakala wa barabara mini na vijijini (Tarula) wahakikishe kuwa wanawasimamia vizuri wakandarasi waliotia saini mikataba kwaajiri ya ujenzi wa miundombinu ya barabara mkoani humo pia wakandarasi wametakiwa kufanya kazi kwa uaminifu Zaidi wakitambua kuwa fedha hizo ni za walipa kodi ambao wengi wao wenye vipato vya chini.

Kwa upande wao baadhi ya wakandarasi ambao walihudhuria afla hiyo ya utiaji saini mikataba kwaajiri ya ujenzi wa miundombinu ya barabara wameishukuru serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa jitihada zinazofanywa ya kuhakikisha kuwa miundo mbinu ya barabara inatengenezwa kutoka mjini mpaka vijijini jambo ambalo linapelekea wakulima kuweza kusafirisha mazao yao kutoka mashambani hadi majumbani mwao kwa urahisi zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed akikata utepe kitabu cha utiaji Saini mikataba ya miundombinu ya barabara mkoani Ruvuma yenye thamani ya Tsh. Bilion22.1
Please follow and like us:
Pin Share