Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Gairo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Gairo mkoani Morogoro tarehe 02 Agosti, 2024. Mhe. Rais Samia ameanza Ziara ya Kikazi mkoani Morogoro ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi.
Shamrashamra za Wananchi wa Gairo mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwasili katika Wilaya hiyo kwa ajili ya kuwahutubia tarehe 02
Agosti, 2024