Na Isri Mohamed

Kiungo wa kimataifa wa Yanga, Stephanie Aziz Ki amebeba tuzo nne usiku wa kuamkia leo katika hafla ya ugawaji tuzo ya wanamichezo bora wa soka kwa msimu uilopita 2023/24 iliyoandaliwa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).

Katika tuzo hizo ambazo zimefanyika katika ukumbi wa Superdome Masaki jijini Dar es Salaam, Aziz Ki aliyekuwa kwenye vipengele vyenye mchuano mkali, ameshinda tuzo ya mfungaji bora akiwa na magoli 21 ya ligi kuu.

Tuzo ya pili aliyoshinda Aziz ni ya kiungo bora akiwashinda Kipre Junior wa Azam Fc na Feisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam Fc.

Aidha nyota huyo kutoka Burkinafaso ametwaa tuzo ya kikosi bora cha mwaka ambacho pia kimeingiza wachezaji wengine ambao ni hawa wafuatao.

Lay Matampi (Coastal Union),
Kouassi Yao (Yanga SC),
Mohamed Hussein (Simba SC),
Ibrahim Bacca (Yanga SC)
Dickson Job (Yanga SC)
Feisal Salum (Azam FC)
Mudathir Yahaya (Yanga SC),
Kipre Junior (Azam FC), Aziz Ki (Yanga SC),
Maxi Nzengeli (Yanga SC) na
Wazir Junior (KMC).

Tuzo ya mwisho aliyoshinda Aziz ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na watanzania ni ile ya mchezaji bora wa mwaka (MVP) aliyokuwa akichuana na Kipre JR wa Azam fc, Golikipa Djigui Diarra wa Yanga, Feisal Salum wa Azam FC, Golikipa Ley Matampi wa Coastal Union, Mabeki Yao Attouhla na Ibrahim Bacca wa Yanga pamoja na beki Mohamed Hussein wa Simba.

Please follow and like us:
Pin Share