Rais wa Irani Masoud Pezeshkian anasema ataifanya Israel “ijutie” mauaji ya “uoga” ya Haniyeh, akiongeza kuwa Iran “italinda hadhi ya eneo lake, fahari ya heshima na utu”.

Katika taarifa iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP, rais wa Iran alimtaja Haniyeh kama “kiongozi shupavu”.

Kiongozi huyo wa kisiasa wa Hamas, ambaye yuko Qatar, alikuwa akizuru Tehran kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais wa Pezeshkian.

Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei pia anasema kulipiza kisasi kifo chake ni “wajibu wa Tehran”, akiongeza kuwa Israel – ambayo haijadai kuhusika – ilitoa sababu za “adhabu kali”.