Meli kubwa iliyobeba mizigo ya tani elfu 14 kutoka nchini China imetia nanga katika bandari ya Tanga Kwa mara ya kwanza  ikiwa na shehena za mizigo mbalimbali ikiwemo magari 300.

Meli hiyo ya kampuni ya Seefront Shipping Service Ltd, imebeba magari 300 ya mizigo ambayo yanasafirishwa kwenda nchi za DRC Congo, Zambia, Burundi na Rwanda unatarajiwa kukaa bandarini hapo kwa muda wa siku tatu na kuondoka.

Akishuhudia mapokezi ya meli hiyo, Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile alisema fedha zilizowekezwa katika maboresho ya bandari ya Tanga zimeanza kuonesha mafanikio kwani utendaji kazi katika bandari hiyo umekuwa ni wenye  tija.

“Shughuli hii ya leo maana yake ni matokeo ya uwekezaji mkubwa wa maboresho, shehena zimeongezeka mara dufu kutoka shehena 470 mwaka 2019 na kufikia milioni 1 ya sasa, lakini pia meli zimeongezeka kutoka 118  mwaka 2019 hadi 307 mwaka huu,

Please follow and like us:
Pin Share