Mama Mzazi wa Mbunge Halima Mdee, Theresia Mdee, amefariki dunia leo Julai 30, 2024 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mama Mdee alilazwa katika Hospitali hiyo mara kadhaa kwa matibabu ambapo mara ya mwisho kabla ya umauti kumfika alikuwa amelazwa Hospitalini hapo kwa muda wa wiki tatu mfululizo.

Viongozi mbalimbali wamewahi kumtembelea kumjulia hali akiwemo Rais Samia ambaye alifika kumjulia hali Hospitali Februari 01, 2024 akitanguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alimtembelea Januari 30,2024 na Spika wa Bunge alimtembelea Januari 31,2024.

Maziko yake yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo nyumbani kwao Moshi Vijijini.