Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Ibrahim Michael  Mhona akizungumza jambo  leo Julai 29, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani  wakati wa ufunguzi  wa Mazoezi ya medani, Umoja 2024 wanaoshiriki JWTZ pamoja na  Jeshi la Ukombozi la watu wa China kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 60 ya JWTZ pamoja na Ushirikano na Nchi ya China.

Msaidizi Mkuu wa Majeshi, Jeshi la Ukombozi la watu wa China Meja Jenerali Ye Dabin akizungumza jambo leo Julai 29, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani  wakati wa ufunguzi wa  Mazoezi ya medani, Umoja 2024 wanaoshiriki ni JWTZ pamoja na  Jeshi la Ukombozi la watu wa China kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 60 ya JWTZ pamoja na Ushirikano na Nchi ya China.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda akipewa maelezo ya ufanisi wa Silaha za kivita za Jeshi la Ukombozi la watu wa China  katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Jeshi la Ukombozi la watu wa China wakiwa katika picha ya pamoja.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika picha ya pamoja.

Makomando wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani  katika ufunguzi wa  Mazoezi ya medani, Umoja 2024 na Jeshi la Ukombozi la watu wa China 

…………………………………

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda amefungua mazoezi ya medani, Umoja 2024 yanayoshirikisha  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Jeshi la Ukombozi la watu wa China ikiwa ni sehemu ya Maadhimisha Miaka 60 ya JWTZ pamoja na Ushirikano wa  Jeshi la Ukombozi la watu wa China.

Akizungumza leo Julai 29, 2024 Mkoani Pwani katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo wakati akifungua Mazoezi ya Medani, Umoja 2024, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, amesema kuwa ni muhimu kushirikiana katika utendaji kazi, huku akieleza wanatambua juhudi za Jeshi la Ukombozi la watu wa China kwa kujenga vituo vya jeshi pamoja na kutoa vifaa.

Jenerali Mkunda amesema kuwa mazoezi ya pamoja ni muhimu kwa jeshi kwani inawakumbusha ushirikiano wa kimataifa.

“Mazoezi haya yana tukumbusha kupambana na majanga ya dunia ikiwemo usafirishaji wa dawa za kulevya pamoja na binadamu” amesema Jenerali Mkunda.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona, ameishukuru Serikali ya Tanzania na China kwa kufanikisha  mazoezi ya medani, umoja 2024.

Mazoezi ya Medani, Umoja 2024 yatafanyika kwa muda wa siku 14 kuanzia leo  katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Jeshi la Ukombozi la watu wa China watafanya mazeozi ya pamoja kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.