Kuelekea kilele cha siku ya Mwananchi Agosti 04, 2024, klabu ya Yanga imetangaza kucheza na klabu ya Red Arrows kutoka nchini Zambia

Akizungumza na wanahabari mapema leo katika ofisi za Yanga, Afisa muhamasishaji Haji Manara amesema Red Arrows ambao ni Mabingwa wa Michuano ya KAGAME Cup watawasili nchini hivi karibu kwa ndege yao binafsi kwa ajili ya sherehe hizo zitakazofanyika katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

“Champion wa Kagame Cup msimu huu, Red Arrows kutoka Zambia ndio timu tutakayocheza nayo siku ya Tarehe 4, pale Benjamin Mkapa Stadium na wametuambia watakuja na Ndege yao ya Jeshi,” amesema Manara.

Please follow and like us:
Pin Share