Na Lookman Miraji, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Kundi la kwanza la Timu ya Tanzania itayoshiriki Michezo ya Olimpiki nchini Ufaransa limewasili salama jijini Paris asubuhi ya jana.
Kundi hilo la kwanza lina waogeleaji wawili, Sophia Anisa Latiff na Collins Phillip Saiboko na mwalimu wao Alexander Harrison Mwaipasi pamoja na Daktari wa timu, Dkt Eliasa Abdallah Mkongo.
Waogeleaji wataanza Mashindano Julai 30, ambapo Collins Phillip Saiboko atashindana katika michuano ya mita 100 Freestyle kwa wanaume.
Sophia Anisa Latiff atashindana Agosti 3, michuano ya mita 50 freestyle kwa wanawakr
Mwingine aliyewasili hapo jana jijini Paris ni mwalimu wa mchezo wa Judo, Innocent John Mallya,
ambaye mchezaji wake, Andrew Thomas Mlugu (Kg 73), tayari yupo Paris kwa mwaka katika kambi maalumu ya mazoezi ya CRJ Centre iliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC).
Andrew Thomas Mlugu ataamza kushindana Agosti 2.
Wanamichezo wanne, ambao wote ni wakimbiaji wa Marathon, bado wako kambini Arusha wakijifu. Wanatarajiwa kuwasili Paris Augosti 7 na Marathon itakuwa Agosti 11.
Wanariadha hao wa Marathon ni Wanaume wawili, Alphonce Felix Simbu na Gabriel Geay, na wanawake wawili Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri.