Makamu wa Rais,Kamala Harris ameonekana kuungwa mkono na wajumbe wa kutosha wa Chama cha Democratic kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama hicho.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Habari la Associated Press umegunduakuwa zaidi ya wajumbe 1,976 wako tayari kupiga kura ya ndio katika Kongamano la Kitaifa la Kidemokrasia (DNC).
Hatahivyo taarifa zinasema kuwa uidhinishaji huo sio rasmi kisheria, lakini ikiwa jumla ya wajumbe watamuunga mkono Harris kuanzia sasa hadi siku ya kupiga kura basi kuna uwezekano mkubwa wa kushinda.
Mpaka sasa wajumbe kutoka angalau majimbo 27 wamekiri kumuunga mkono Kamala Harris huku uchaguzi huo ukipangwa kufanyika Agosti mosi hadi Agosti 7.
Utafiti huu ni dalili ya msingi wa kumuunga mkono Kamala Harris baada ya Rais Joe Biden kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho siku ya Jumapili.