Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Kiteto

Mwenge wa uhuru Kitaifa umetua Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara na kupitia jumla ya Miradi 14 ya thamani ya zaidi ya bil.3,376,948,330.0,

Hayo yalibainishwa Julai 17,2024 na Mkuu wa Wilaya hiyo Remidius Mwema Emmanuel wakati akitoa taarifa yake ,bele ya Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange na kiongozi wa ,bio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava.

Emmanuel amesema Mwenge wa uhuru ukiwa katika Wilaya hiyo utakimbizwa katika umbali wa km. 67 kuanzia eneo la mapokezi hadi eneo la mkesha,

“Mwenge wa uhuru umepita katika tarafa 2, kata 4, Vijiji 5 na kukimbizwa umbali wa km.67, ambapo jumla ya Miradi 14 inatarajia kufikiwa na Mwenge wetu wa uhuru” amesema Emmanuel.

Aidha amesema kati ya miradi hiyo mradi mmoja umezinduliwa, miradi 3 imegunguliwa na miradi 10 imekaguliwa.

“Thamani ya miradi hiyo yote ni sh.bil.3,376,948,330.01, ambapo kati ya fedha hizo jamii imechangia mil.4, Halmashauri ya Wilaya imechangia sh. 66,990,000 huku Serikali Kuu ikiwa imechangia bil.3,305,958,330.01” amesema Mkuu huyo.

Aidha Mkuu huyo amefafanua kuwa wananchi wa Wilaya ya Kiteto katika Mbio za Mwenge wa uhuru Mwaka 2024 wamechangia jumla ya ah.mil.69,769,500, vitu mbali mbali N’gombe 4 na mbuzi 4, wenye thamani ya sh.mil.1.6.

” Kati ya fedha hizo sh.mil.67,769,500 zimetumika kugharamia manunuzi ya vifaa kwaajili ya watu wenye mahitaji malum ambayo vimekabidjiwa kwa wahusika na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa eneo la mapokezi

Please follow and like us:
Pin Share