Ikulu ya Marekani White House imesema rais wa taifa hilo, Joe Biden amegundulika kuwa na virusi vya UVIKO-19 na kuonesha dalili za athari za wastani za virusi hivyo.

Msemaji wake, Karine Jean-Pierre amesema Biden aliyekuwa tayari amepata chanjo hiyo na kadhalika ile ya kuongezewa nguvu alijihisi hali isio njema baada ya maambukizi hayo.

Hali hiyo ilimfika wakati kiongozi huyo, ambaye anasaka kuchaguliwa tena Novemba, akiwa anafaya kampeni huko Nevada.

Alikutana na wafuawasi mapema Jumatano lakini alikatisha hotuba yake katika jimbo hilo ambalo lina nguvu sawa za ushawiwishi kati ya chama chake cha Democrats na kile cha Republican.

Hata hivyo Ikulu ya Marekani imesema Biden atarejea katika makazi yake ya kibinafsi huko Delaware ambapo atajitenga huku akiendelea kutekeleza majukumu yake yote kikamilifu wakati huo.