Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Namtumbo
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Juma Pandu ameiomba Serikali kuona umuhimu wa kuligawa jimbo la Namtumbo ili wananchi waweze kupata huduma mbalimbali kwa urahisi tofauti na hivi sasa jimbo hilo lina kata 21 ambalo kijografia kata zake zimekaa mbali na makao makuu ya halmashauri hiyo ambalo linapakana na Wilaya ya Tunduru,Mkoa wa Morogoro na Nchi jirani ya msumbiji.
Pandu ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mkongo Nakawale amesema kuwa kwa ujumla hali ya wananchi ambao wanahitaji kupata huduma ya halmashauri wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa namna ya kufika makao makuu ya Halmashauri .
Alisema kuwa kwa wakzi wa maeneo za kata ya Magazini na Lusewa ambako ambazo zipo umbali wa kilomita Zaidi ya 280 hadi makao makuu ya Wilaya wamekuwa wakishindwa kusafiri au kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo kwenye kata zao kutokana na umbali uliopo na miundombinu ya barabara hasa kipindi cha masika inakuwa mibovu.
Pandu alifafanuwa kuwa kutoka kata ya kitanda hadi makao makuu ya wilaya ya namtumbo kuna umbali wa Zaidi ya kilomita 150 jambo ambalo limekuwa likisababisha shughuli mbali mbali za maendeleo kuto tekelezwa kwa wakati kutokana na miundo mbinu ya barabara kuwa mibovu.
“zipo jitihada zimefanywa za kuiomba srikali ione umuhimu wa kuligawa jimbo ambalo ni kubwa sanahivyo nina imani serikali itaweza kusikiliza kilio cha wananchi wa jimbo la Namtumbo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiomba jimbo hilo ligaiwe”alisema Pandu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Namtumbo Zuberi Lihui akizungumza na waandishi wa habari katika Kijiji cha Mputa alisema kuwa Jimbo la Namtumbo ni kubwa sana itakuwa ni vyema kuona umuhimu wa kuligawa ili kupunguza changamoto zilizopo na alilifananisha kuwa Jimbo la Namtumbo linafanana ukubwa na mkoa wa wa Mtwara ambako kuna majimbo mengi tofauti lilivyo jimbo la Namtumbo ambalo linaendelea kuwahudumia wananchi katika mazingira magumu.
Lihui alisema kuwa endapo serikali itakubali kuligawa jimbo la Namtumbo Wilaya ya Namtumbo itakuwa na maendeleo Zaidi kwa sababu wananchi watakuwa wanapata huduma kiurahisi tofauti na ilivyo sasa ambako kuna changamoto nyingi ambazo Mbunge aliyopo madarakani Vita Kawawa anajitahidi kuzitatua lakini bado zingine zinachelewa kupatiwa ufumbuzi kutoka na jiografia ya maeneo ya Jimbo hilo.