Na Isri Mohamed
Aliyekuwa kocha wa klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Rhulan Mokwena anatarajiwa kutambulishwa kuwa Kocha mkuu wa Wydad Athletic Club ya nchini Morocco.
Kocha Rhulan ambaye anakwenda kuchukua mikoba ya Aziz Ben Askar, tayari ameshatua nchini humo na kufanya makubaliano na Wydad na muda wote kuanzia sasa atatangazwa rasmi.
Wydad ambayo msimu uliopita wamemaliza nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu ya Morocco, wamepania kurudisha ufalme wao nchini kwao na kwenye ligi ya mabingwa Afrika ambayo waliishia hatua ya makundi tu msimu uliopita.
Mokwena alijiunga na Mamelod Sundowns mwaka 2020, akiwa kocha msaidizi na baadaye mwaka 2022 akapandishwa kuwa kocha mkuu, ambapo ameisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Afrika Kusini kwa misimu minne mfululizo, na kombe la African Super League.