Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo, ametoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi ya dawa na kuacha kutumia kiholela na badala yake wafuate ushauri wa daktari.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Fimbo amesema kuwa Mamlaka hiyo inaendelea kupambana na usugu wa vimelea vya Dawa na kuelimisha jamii katika kuhakikisha Dawa zinatumika kwa ufasaha na usahihi kwakufuata maelekezo sahihi ya Kitaalam.

“Usugu wa Dawa umekuwa ukiongezeka siku hadi siku kutokana na matumizi ambayo sio sahihi, nakupelekea wananchi wengi kupata madhara” amesema.

Amesema TMDA imeshiriki maonesho ya Sabasaba mwaka huu ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya Dawa na kufahamu majukumu ya Taasisi hiyo.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutembelea kwenye banda lao kupata elimu ya udhibiti na matumizi sahihi ya Dawa awa na vitenganishi.

Please follow and like us:
Pin Share