Na Helena Magabe,JamhuriMedia, Mara

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amefurahishwa na hatua ya Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa habari Mara(MRPC )Mugini Jacob kuazisha mchakato wa tuzo ya uandishi ulio Bora bora Mara.

Haya ameyasema Julai 5, 2024 katika mdahaho wa Mara bora kwa uwekezaji na kuishi uliohusisha waandishi wa habari wa Mara pamoja na wadau mbali mbali wa habari ambapo amesema uazishaji wa tuzo hizo itakuwa na chachu kwa aandishi wa habari wa ndani ya Mkoa wa Mara na nje uma wa Tanzania mambo mazuri yanayopatikana Mara pekee.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mara na mwaandaji wa mdahalo huo Mugini Jacob amesema kuwa kila mwisho wa mwaka zitatolewa tuzo za uandishi bora ambapo mshindi wa kwanza atapokea shilingi milioni moja na cheti.

Amesema habari hizo zitakuwa ni za kilimo, ufugaji, madini, utalii, uhifadhi, ujenzi, miundombinu, uhifadhi wa wanyamapoli,uvuvi endelevu pamoja habari za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wadau mbalimbali walioshiriki ni pamoja Barrick North Mara Gold mine, Nyihita sunflower, TCCIA,WAMACU,TANROAD, Haippa plc,Grumeti reserves pamoja na Grumeti fund ambao walitoa elimu nzuri Kwa waandishi kuhusiana na sekta zao.

Mkurugenzi wa kiwanda mafuta ya Alizeti Nyihita Wilfred alisema Kwa siku kiwanda chake kinazaluza tan 24 mafuta na Kwa mwaka ni tan 8,700 ila kwa Sasa kuna changamoto ya uzalishaji ameshauri wadau kuwekeza kwenye kilimo Cha alizeti,maharage,kahawa na mazao mengine kwani mkoa una ardhi ya kutosha pia unafaa Kwa uwekezaji na kuishi David Mwakipesile toka Grumeti alitoa elimu ya maguu hatari na mengineyo .

Waandishi nao walitumia fursa hiyo kumpongeza Mugini Jacob Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi Mara na kumtabilia mambo makubwa mbeleni miongoni mwao ni Waitara Meng’anyi pamoja na Maximilian Ngesi mwandishi wa habari Mstaafu ambaye alisema Kwa muda mfupi tu aliochaguliwa Jacob amefanya jambo kubwa mbeleni atakuwa Mtu mkubwa sana.

Please follow and like us:
Pin Share