Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,Dar es Salaam

WANANCHI na wadau mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kutembelea Banda la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika ya Mashariki (EACOP) kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maraarufu ‘Sabasaba’ yanayofanyika viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Kupitia maonesho hayo, EACOP imepata fursa ya kutoa elimu kwa wananchi na wadau kuhusu masuala mbalimbali yanayotekelezwa na mradi ikiwemo namna mafuta hayo ghafi yatakavyosafirishwa kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Pwani ya Chongoleani mkoani Tanga.

“Nina hamu kubwa sana ya kuzifahamu fursa zilizopo kwenye eneo la mradi na jinsi unavyotekelezwa. Kiasili mimi natokea katika Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma na mkazi wa Yombo Vituka Wilaya ya Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Ezekiel Lubuva.

Lubuva ambaye pia ni mfanyakazi katika Kituo cha Mafuta alisema aliamua kutembelea banda la EACOP lililopo TPDC ‘Square’ kupata taarifa sahihi kuhusina na mradi pamoja na kuzifahamu fursa zilizopo kwenye mradi katika kubadilisha maisha ya watu.

Mradi EACOP utekelezaji wake upo katika eneo urefu wa kilometa 1,147 ndani ya Tanzania na kilomita 296 nchini Uganda na kufanya jumla ya kilomita 1,447. Mradi umepita katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara and Tanga zikiwemo wilaya 24,kata 134 na vijiji zaidi 180.

“Nimeweza kujua kuwa watu zaidi ya 13,161 walipitiwa na mradi wameshapata fidia zao kwa namna mbalimbali ikiwemo kujengengewa nyumba, kulipwa fedha na mafao mengineyo kama fidia,” alisema Bw Lubuva.

Manyangu Madoshi anayetokea Shinyanga miongomi mwa waliotembelea banda hilo alionyesha furaha yake kuhusu mradi kwani alisema umetengeneza ajira nyingi kwa watanzania na hasa kwa wakazi waliopo maeneo yanayopitiwa na mradi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa EACOP(Tanzania), Catherine Mbatia amesema wananchi wengi wanaotoka mikoa minane inayopitiwa na mradi na wanaishi hapa Dar es Salaam na maeneo mengine wamekuwa na shauku kubwa.

“Tumekuwa tukiwaelimishwa kuwa bomba hilo litafukiwa chini ya ardhi na baada ya kufukiwa binadamu na wanyama wataendelea na maisha yao kama kawaida,” alisema Mbatia na kuongeza maonesho imekuwa nzuri ya kutoa elimu kuhusu faida za mradi.M

batia amesema wamewezakujifunza namna mradi unavyotoa fursa za ajira kwa wananchi wa Tanzania na Uganda wakiwemo watoa huduma za ndani , kuwezesha mapato kwa nchi wenyeji, uboreshaji wa miundombinu pamoja na faida nyingine.

EACOP Ltd ni kampuni yenye madhumuni maalum, inayosimamiwa na Mkataba wa Wanahisa wake ambao ni TotalEnergies wahisa 62, Uganda National Oil Company (UNOC) wahisa 15, Shirika la Maendeleo Tanzania (TPDC) wanahisa 15 na Kampuni ya Kichina ya CNOOC wanahisa 8 .

Maonesho hayo ‘Sabasaba’ yalifunguliwa hivi karibuni na Rais Mhandisi Dk Filipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji aliyeambatana na mwenyeji wake Rais Dk Samia Suluhu Hassan aliyewataka washiriki kuyatumia maonesho hayo sehemu yakujenga na kuimarisha mahusiano ya kibishara.