Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema baadhi ya wananchi waliohojiwa na tume inayotayarisha Dira ya Taifa 2050 wametaka suala la kuboresha huduma za afya liwe kipaumbele.
Prof. Mkumbo ameyasema hayo leo Julai 06, 2024 wakati akifungua Kongamano la wadau wa Sekta ya Afya kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 lililoandaliwa na Wizara ya Afya kwa wadau wake.
“Mhe. Waziri Ummy mimi nikushukuru sana kwakuwa Sekta ya kwanza kuandaa kongamano na kutualika kuja kuchukua maoni ya wadau wenu, ninyi kama sekta ndio mnawajua vilivyo wadau wenu” amesema Mhe. Prof. Kitila na kuongeza:
“Kuwaleta wadau wenu kutatupatua uga wakukusanya kile ambacho ninyi kama wadau mnakiona kwa maslahi mapana ya Taifa tunapoelekea Diara ya Taifa 2050” amesisitiza Prof. Kitila
Profesa Mkumbo amesema, wananchi waliohojiwa katika hatua za awali walisema Serikali imejidhatiti kuweka miundombinu ya afya na lililosalia sasa inatakiwa kuboresha huduma za Afya.
Awali akitoa Salaam za Ofisi ya Rais TAMISEMI, Naibu Waziri anaye shughulikia Afya, Dkt. Festo Dugange, ameiomba kamati hiyo kuzingalia suala lakuboresha huduma za Afya katika ngazi ya msingi.
“Dira ya Taifa 2050 ilenge Kuimarisha Huduma za Kibingwa na Ubingwa Bobezi hadi ngazi ya Wilaya ili kupunguza mzigo kwenye Hospitali za Mikoa na Kanda” amesema Mhe. DKT. Dugange
Kongamano la kitaifa la wadau wa Sekta ya Afya limeandaliwa na Wizara ya Afya na kuwaalika wadau wake kwa ajili yakutoa Maoni itakayowezesha kuingizwa kwenye Dira ya 2050 kwa mustakabali wa Afya za watanzania.