Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifa Hamis ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) ili kuona fursa mbalimbali za uwekezaji zinatopatikana kupitia nchi 26 zilizoshiriki.
Ameyasema Julai 04, 2024 jana jijini Dar es Salaam katika mkutano maalumu wa wafanyabiashara wa Tanzania na Japan uliokuwa na lengo la kutafuta fursa za wafanyabiashara wa Japan kuwekeza nchini.
Latifa amebainisha kuwa mkutano huo umehudhuriwa na kampuni tisa katika sekta mbalimbali kama uvuvi, afya, teknolojia, kilimo na usafirishaji ambazo zimekuwa zikionesha fursa za uwekezaji zilizopo.
“Nichukue fursa hii kuwaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi katika maonesho haya kwa kuangalia fursa mbalimbali zinazotolewa na nchi zilizoshiriki maonesho pamoja kujifunza mambo mbalimbali,” amesema Latifa.
Kwa upande wake balozi wa Japan nchini, Yasushi Misawa amesema amevutiwa na maonesho hayo kwani yanawapa fursa ya kujifunza vitu vingi kutoka Tanzania.
Kwa upande wake balozi wa Japan nchini, Yasushi Misawa amesema amevutiwa na maonesho hayo kwani yanawapa fursa ya kujifunza vitu vingi kutoka Tanzania.
“Maonesho haya ni mazuri sana kwani yanatupa fursa ya kujifunza kutoka Kwa Watanzania na wao watajifunza kutoka kwetu kwani kuna vitu tunavyo na Tanzania havipo na vingine wanavyo na sisi hatuna.
“Ushirikiano wetu wa miaka mingi tunahitaji uendelee kuwepo kuimarisha uchumi wa nchi zetu,” amesema