Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia
Dar es Salaam
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo Martini Mbwana ameacha kitendawili kwa wafanyabishara suala la kufunga na kufungua maduka ni maamuzi yao baada ya kuwapatia mrejesho wa kikao walichozungumza baina yao na viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba .
Kitendawi hiko amekiacha leo Juni 26, 2024 Jijini Dar es Salaam katika mkutano mkubwa na Wafanyabishara hao Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku 3 tangu wagome kufungua maduka yao wakilalamikia Mamlaka ya mapato TRA kuwapa usumbufu wa kimbiza kimbiza kila kona kutoza kodi faini na kuwasababishia baadhi ya wateja wao kuhama na baadhi yao mitaji yao kuelekea kufilisika.
“Niseme ukiona mfanyabiashara amefunga duka lake na kuamua kukaa nje ujue amevurugwa hivyo isitumike nguvu kubwa kwa kutumia maneno makali kinachotakiwa ni kuka meza moja na kuzungumza kujua tatizo linalosababisha hadi akachukua maamuzi magumu hivyo hii ni mara ya pili hali hii kutoke na tukaahidiwa lakini haikutekelezwa na sasa hivyo tunaomba Serikali ifike mahali Kodi zote zitozwe kwa pamoja na ziishie bandarini ” amesema Martini.
Mbwana ame amefafanua kuwa mwaka huu walikaa kikao Anatoglo lakini hakuna muafaka aliishia kuitwa mara nne kituo cha polisi kuhojiwa lakini hakukata tamaa kudai haki na kile wanachotendewa hivyo sasa kikao alichoitiwa Dodoma wamekaa meza moja na kuzungumza na ahadi imetolewa kero zao zinakwenda kutatuliwa hivyo amewaachia Wafanyabiashara hao uamuzi wa kuamua kufunga maduka au kufungua ni juu yao kwani funguo humiliki wao.