Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifasi Bisanda amekanusha kuvuja kwa mitihani na kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu wakati wa mitihani cmya muhula uliopita.
Aidha pia ameonya kwa wale wote wenye nia ovu ya kujaribu kufanya vitendo vya udanganyifu kwa kuwafanyia mitihani wanafunzi wa chuo kwenye mitahani yao.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini dar es Salaam leo Juni 28 2024, alipokuwa akitoa taarifa juu ya matukio ya siku za hivi za karibu, ambapo amesema walifanikiwa kuwakama watu waliojifanya wanafunzi na watahiniwa wa kwa lengo la kuwafanyia mitihani wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.
Bisanda amesema kuanzia Juni 3 hadi 24 mwaka huu, wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wapatao 10417,waliandika mitihani yao katika vituo 53 vya mitihani, ikiwa ni pamoja na Zanzibar.
Mkuu huyo amesema uongozi wa chuo ukishirikina na maafisa wa usalama wa Taifa walibahini mbinu hizo chafu ambapo amedai watuhumiwa 17 walijaribu kutaka kuingia kwenye vyumba vya mitihani wakiwa na lengo la kufanya mitihani kwa kutumia vitambulisho na majina ya watahiniwa wa chuo hicho, ndipo walipobaini sura zilipo kwenye vitambulisho havifanani na wahusika
Kwa upande mwingine Bisanda amesema kuwa kwa kipindi cha miaka zaidi ya miaka 15 chuo hicho hakijawahi kukumbwa na matukio ya aina hiyo jambo ambalo ameelezea wamelazimika kulitolea ufafanuzi huku akionya vikali wale wote wanaofikiria chuo hicho ni kichochoro, cha kufanya udanganyifu ili kujipatia vyeti vya taaluma vinavyotolewa na chuo hicho kwa namna yoyote.
Vilevile Profesa Bisanda amesema chuo hicho kimekuwa kikijizolea sifa kitaifa na Kimataifa,kwa kuwa na mfumo madhubuti wa usalama wa mitihani yake, ambapo amesisitiza kuwa chuo kimeweza kutumia wataaalam wao wa Tehama,kujenga mfumo wa mitihani ambapo amedai ni vigumu sana kuvuja kwa mitahani chuoni hapo.
Kwa sasa watuhumiwa hao wapo mikononi mwa vyombo vya dola huku akiahidi swala hili kulipeleka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Camilius Wambura kwa hatua zaidi na akaenda mbali zaidi kufika hadi Ofisi ya Rais, kwa ajili ya Utekelezwaji zaidi wa swala hlilo huku Uchunguzi ukiendelea.
Alipolizwa hatma ya wanafunzi walioshiriki kufanya vitendo hivyo hatua gani itachukuliwa amesema uchunguzi bado unaendelea na utakapobainika wahusika wote watafikishwa kwenye kamati ya nidhamu ya chuo kwa ajili hatua zaidi za kinidhamu.
Pia ametoa onyo kali kwa wale wote wanata kufanya udanganyifu ikiwemo kuvujisha mitihani au hata kuwafanyia mitihani watahiniwa wa chuo hicho kuacha mara moja, huku akiahidi kufungua mifumo ya TEHAMA ili kuzuia vitendo vya aina hiyo chuoni hapo.