NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk Mohamed Said Dimwa amesema wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu (NEC) CCM Taifa Zanzibar wamepitisha pendekezo la kuishauri Kamati Maalumu ya NEC kuridhia kumuongezea muda Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi wa kuongoza muhula wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka saba badala ya mitano.
Alisema hayo wakati akifunga mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya uliofanyika katika ofisi za wilaya hiyo Kiembesamaki. Dk Dimwa alieleza kuwa maamuzi ya kumuongezea muda wa kuongoza Dk Mwinyi yanatokana na kuridhishwa na kasi yake ya kiutendaji katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 20202025 kwa zaidi ya asilimia 100 ndani ya kipindi miaka mitatu na miezi kadhaa tangu aingie madarakani.
Katika maelezo yake Dk Dimwa alieleza kuwa CCM Zanzibar imeona serikali kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwani wananchi wanahitaji maendeleo endelevu hivyo Dk Mwinyi anafaa kuongezewa muda ili Zanzibar iwe kisiwa kilichoendelea kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“Wajumbe wa Sektetarieti tumejadili na kutathimini kwa kina juu ya utendaji wa Dk Mwinyi, tukajiridhisha kuwa hakuna mbadala wake na anastahiki aongoza nchi kwa kipindi cha miaka saba ili apate muda mzuri wa kufanya mapinduzi ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi na kijamii