Mamlaka nchini Saudi Arabia imetangaza kuwa idadi ya mahujaji waliokufa kutokana na joto kali wakati wa Hijjah ya mwaka huu imefika watu 1,300 na kwamba asilimia 83 ya waliokufa walikuwa mahujaji ambao hawakusajiliwa.
Miongoni mwa raia wa Misri 658 waliokufa wakati wa kuhiji, 630 walikwenda Makkah lakini hawakusajiliwa.
Rais Abdel Fattah El-Sisi alimwamuru Waziri wake mkuu Moustafa Madbouly kuchunguza kiini cha mkasa huo.
Takriban nchi 10 ndizo zimeripoti vifo vya raia wake walioshiriki moja ya nguzo tano za Uislamu ambayo waumini wote wenye uwezo wa kiafya na kifedha ni lazima wakamilishe angalau mara moja maishani mwao.