Wanawake 24 wa Sudan wameshtakiwa kwa kujivunjia heshima, baada ya kuonekana wamevaa suruali katika karamu moja mjini Khartoum.
Karamu hiyo ilivamiwa na polisi wa nidhamu siku ya Jumatano.
Suruali zinachukuliwa na wakuu kuwa vazi la utovu wa adabu, na adhabu yake ni mijeledi 40 pamoja na faini.
Wanaharakati wanasema maelfu ya wanawake wanakamatwa kila mwaka, na kuichapwa mijeledi.
Wanasema sheria inayopiga marufuku suruali na sketi fupi na za kubana, inawabagua wakristo, na inatumiwa kiholela.
Kawaida wanaweke nchini Suana huvaa nguo ndefu.
Wanawake 24 Sudan Hatarini Kucharazwa Viboko 40 Kila Mmoja
Jamhuri
Comments Off on Wanawake 24 Sudan Hatarini Kucharazwa Viboko 40 Kila Mmoja