Takriban watu 34 wamekufa baada ya kunywa pombe yenye sumu katika jimbo la Tamil Nadu, kusini mwa India, maafisa wamesema.
Kisa hicho kilitokea katika wilaya ya Kallakuruchi ambapo wakazi kadhaa waliugua baada ya kunywa pombe hiyo Jumanne usiku.
Takriban watu 80 wanatibiwa katika hospitali kutokana na magonjwa kama vile kuhara kupita kiasi na maafisa wanasema idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi.
Watu wawili wamekamatwa hadi sasa na uchunguzi zaidi unaendelea.
Mamlaka pia imemsimamisha kazi afisa mkuu wa polisi na wanachama kumi wa mrengo wa utekelezaji wa katazo la serikali – wanaodai usafirishaji wa pombe haramu katika jimbo hilo unatokana na uzembe.
Makumi ya watu hufa nchini India kila mwaka baada ya kunywa pombe ya wauzaji wa pombe kutoka kwa viwandani vya barabarani.
Wauzaji pombe mara nyingi huongeza methanoli – aina ya pombe yenye sumu kali kwenye mchanganyiko wao ili kuongeza nmakali ya pombe.
Ikinwewa kiasi kidogo, methanoli inaweza kusababisha upofu, uharibifu wa ini na hata kifo.