Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema watumishi wa Umma wanapaswa kumuenzi aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro marehemu Tixon Nzunda kwa kuwa waadilifu, wazalendo na kumtanguliza Mungu katika majukumu yao.

Dkt. Mpango amesema hayo wakati akizungumza na waombolezaji alipowasili nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Bi. Grace Mgombela ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda pamoja na familia yake mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia hiyo Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 19 Juni 2024.

Amesema marehemu Nzunda alikuwa kiongozi na mtumishi wa umma muadilifu na makini katika nafasi mbalimbali alizowahi kuzitumikia serikalini.

Amesema serikali imeguswa na msiba huo na inaungana na waombolezaji wote katika kipindi hiki kigumu. Aidha amewashukuru wananchi kwa kujitoa na kuwa pamoja na familia tangu ilipofikwa na msiba huo.

Vilevile Makamu wa Rais amewasihi watanzania kuendelea kuishi vema kazini, kuishi vema na marafiki pamoja na majirani. Amewaasa waombolezaji kupokea msiba huo kama ni mipango ya Mungu na kumuombea marehemu apumzike kwa amani.

Aidha Makamu wa Rais ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Alphonce Edson aliyekuwa dereva wa Marehemu Tixon Nzunda waliofariki pamoja katika ajali ya gari Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Juni Juni 18, 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisali pamoja na familia ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia hiyo Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 19 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waombolezaji mbalimbali mara baada ya kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 19 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waombolezaji mbalimbali mara baada ya kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 19 Juni 2024.
Please follow and like us:
Pin Share