Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Huduma za Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka amesema kuwa kufikia machi 2024 Idadi ya watu ya watumiaji simu janja imeongezeka kufikia asilimia 32.59 kutoka asilimia 32.13 iliyorekodiwa Desemba 2023.

Aidha amesema idadi ya watu wanaofikiwa na utangazaji wa televisheni kwa njia ya setelite (DTH) ni asilimia 100, idadi watu wanaofikiwa na utangazaji na televisheni kutumia miundombinu ardhini (DTI) ni asilimia 56 huku idadi ya visambuzi ni milioni 3.8.

Ameyasema hayo leo Juni 14, 2024 wakati akiwasilisha mada katika kikao kilichowakutanisha Tume Huru ya Taifa Uchaguzi (INEC) na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

Amesema kuwa sera ya habari na Utangazaji ya mwaka 2003 inatambua sekta hiyo kuwa ni sekta ya huduma za jamii nchini kwa kutoa na kupokea habari inatambulika duniani kote kuwa ni moja ya haki za msingi.

Hata hivyo, Mhandisi Kisaka ametoa wito kwa wanahabari nchini kutambua kuwa wana nafasi kubwa ya kuelimisha jamii ili kuweza kushiriki kikamilifu katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini.

“Vyombo vya habari vina ushawishi mkubwa katika jamii ukiona jamii ya sasa wamachozungumza na wanachojadiliana asilimia kubwa kintokana na ushawishi wake vyombo vya habari,” amesema Mhandisi Kisaka.

Amesema kuelimisha wananchi lazima kuwe na,weledi, maadili katika taaluma vizingatiwe ili kuhakikisha umma unajisikia faraja kushiriki katika maboresho hayo bila kusita.

Pia amesema wanaunganisha jamii katika masuala ya kitaifa na kuchochea maendeleo katika jamii.

“Nawataka Wanahabari kutambua kuwa wao ni watoa huduma katika jamii na huduma inayotolewa inatambulika kuwa ni haki ya msingi kiraia na haki ya kila mtu,” amesema.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Patrick Kipangula amesema kutoa habari za kweli ni sahii kwa umma wakati wote wa uchaguzi.

“Kupotosha taarifa zisizo sahihi kunaweza kusababisha hofu, kuchochea, ghasia kupunguza imani ya wananchi kwenye mchakato wa uchaguzi,” amesema Kipangula.

Amesema kanuni na usawa na haki kutoa nafasi sawa kwa wagombea wote na vyama vyote vya siasa pia kufuata kanuni, sheria na maadili ya habari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ( INEC), Mtibora Seleman amesema wanaendelea kushirikiana kwa pamoja katika kusukuma maendelo ya Taifa katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Amesema Tume inaendelea kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwasababu wanapata haki zao za kikatiba.

Please follow and like us:
Pin Share