Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Serikali kwa mwaka 2024/2025 imepanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.35 kiasi hicho kinajumuisha: shilingi trilioni 15.74 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali na gharama nyingine .
Ameyasema Juni 13, 2024 Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba Bungeni Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya Mwaka 2024/ 2025 ambapo amebainisha matumizi ya bajeti hiyo kama ifuatavyo mfuko.Mkuu; shilingi trilioni 11.77 kwa ajili ya mishahara ikiwemo ajira mpya pamoja na upandishaji wa madaraja kwa watumishi; shilingi trilioni 2.17 kwa ajili ya mifuko ya reli.
Pia barabara, maji, REA na TARURA; na ruzuku ya maendeleo ya shilingi trilioni 1.19 kwa ajili ya kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na vyuo vya kati pamoja na Programu ya Elimumsingi na Sekondari bila ada.