Na Joyce Kasiki,Dodoma
CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimetoa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuongeza tija katika utendaji kazi kwa waandishi wa habari hasa kwenye eneo la uhuru wa kujieleza.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo,Makamu Mwenyekliti wa chama hicho Wakili Deus Nyabili alisema haki ya kujieleza na haki ya kuoata habari ni haki muhimu ambayo humwezesha mwandishi wa habari kufanya kazi zake kwa tija kwa mawndeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
“Haki ya kujieleza,kupata habari ni jambo kubwa,lakini pia haki ya kupata habari na kuisambaza pia ni jambo kubwa,hivyo ni wajibu wa TLS kuona kwamba hawa wanaotoa taarifa kwa maendeleo ya nchi,wanakuwa na uwezo wa kutosha ,
“Kwa hiyo tukaona tuandae mafunzo haya kwa ajili ya kukuza uwezo wa waandishi wa habari kwa kuwapa elimu kulingana na mambo yanavyobadilika katika jamii .”alisema Wakili Nyabili na kuongeza kuwa
“Kifungu cha 30 cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinaelezea vizuri juu ya haki ya kujieleza na mipaka yake maana hakuna haki isiyokuwa na mipaka,kwa hiyo tunaangalia namna gani mipaka ile inaweza isitumike kuminya uhuru wa wananhabari katika kutoa habari ambayo inainaweza kuwa chanya au hasi ila waweze kuichakata taarifa sahihi kwa ajili ya maendeleo ya jamii.”
Kwa mujibu wa Wakili Nyabili,anaamini kila mmoja atatoka na elimu ya kutosha ila namna gani ataitumia .
Amewaasa waandishi hao waliopata mafunzo kuyatumia mafunzo hayo kwa kwenda kuwaelimisha wanahabari wengine amvao hawajapata mafunzo hayo ili kwa pamoja waweze kua dina taarifa zitakazoleta tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Awali Mkuu wa Idara ya ufuatiliaji na Tathimini TLS Selemani Mgoni alisema lengo mahsusi la mafunzo hayo kwa wanahabari ni kuwajengea uwezo kuhusu uhuru wa kujieleza kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao.
Mshiriki wa mafunzo hayo Rabecca Clayton kutoka AFM Radio alisema anaamini mafumzo hauo yanakwenda luboresha utendaji kazi wa waandishi wa habari kwa maslahi mapana ya Taifa.