Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma
Kutokana na mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano, Serikali imesema asilimia 67 ya watoto walio umri wa miaka 12 hadi 17 wanatumia mitandao ya kijamii ambapo, kati yao ssilimia 4 wamefanyiwa vitendo vya ukatili na uonevu bila ya ridhaa yao.
Hata hivyo imesema Matumizi ya mitandao hayawezi kuepukika kutokana na mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo mitandao imekuwa ni sehemu ya maisha hasa kwa kizazi cha sasa ambapo imekuwa ikitumika kibiashara, elimu na mengineyo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima ameeleza hayo leo jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kueleza kuwa takwimu hizo ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa kujua kiwango cha ukatili dhidi ya Watoto kupitia mitandao (online child abuse) wa mwaka 2
Kutokana na hayo ameliomba Bunge kupitisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo ya Shilingi 67,905,259,000 ili kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa, Wizara kwa mwaka 2024/25.
Waziri huyo ,”Mheshimiwa Spika,Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuwalinda watoto dhidi ya ukatili mtandaoni ambapo katika kuwalinda watoto tayari Wizara ilizindua Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Mtandaoni tarehe 10,” Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa, ameeleza.
Mbali na hayo amesema Wizara yake inalo jukumu la kusimamia na kuratibu maendeleo ya mtoto pamoja na upatikanaji wa haki za msingi kwa mtoto kama zilivyoainishwa katika Mikataba ya Kimataifa, Kikanda na Kitaifa, Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008 na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2019.
“Haki za mtoto ni pamoja na kuishi, kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili, kuendelezwa kupitia vipaji na elimu, kushiriki katika masuala yanayomhusu kulingana
na umri wake na kutobaguliwa kwa namna yoyote ile, ” smesema.
Waziri Gwajima amefafanua kuwa kila mtoto anahitaji malezi yenye kuzingatia haki na mahitaji yake ya msingi hasa katika kipindi cha umri wa miaka 0-8 ambapo ubongo hukua kwa asilimia 90.
” Nguvu kubwa bado inahitajika ili kuhakikisha mtoto anakua na kufikia utimilifu wake na hatimaye kuja kuwa nguvu kazi yenye tija kwa Taifa, “amesema Waziri huyo mwenye dhamana ya Maendeleo ya Jamii nchini.
Licha ya yote hayo Waziri huyo ameeleza kuwa baadhi ya watoto wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na malezi duni na vitendo vya ukatili kutoka kwa ndugu wa karibu, familia na jamii inayowazunguka.
“Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta imeendelea kuboresha mifumo ya kisheria ili kuimarisha ulinzi na usalama wa mtoto kwa kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Mtoto, Sura ya 13, Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 na Sheria ya Makosa ya Mtandao, Sura ya 443 kwa lengo la kumlinda mtoto nje na ndani ya Mtandao, “amesisitiza.
Amesema Wizara inaendelea kurekebisha Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za mwaka 2012, Kanuni za Makao ya Watoto za mwaka 2012, Kanuni za Uasili Watoto za mwaka 2012 na Kanuni za Malezi ya Kambo za mwaka 2012 ili kuhakikisha mazingira ya malezi ya mtoto wa kitanzania ni salama kwa makuzi stahiki.
Kuhusu waliojifungua watoto kabla ya siku zao kutimia (njiti) Wizara inashirikiana na Wizara nyingine za kisekta kwenye kuboresha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 lengo likiwa ni kuweka vifungu vya kumuongezea muda mama aliyejifungua mtoto njiti ili kuweza kupata muda wa kutosha wa kumhudumia mtoto vizuri tofauti na sheria ilivyo kwa sasa.