JamhuriComments Off on DCEA yakamata kilo milioni moja dawa za kulevya
Na Mwandishi Wetu, JakhuriMedia, Dodoma
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola imefanikisha kukamata jumla ya kilogramu milioni 1.96 za dawa za kulevya mwaka 2023.
Katika ukamataji huo, watuhumiwa 10,522 kati yao wanaume 9,701 na wanawake 821 walikamatwa na Mamlaka hiyo.
Katika taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema dawa za kulevya zilizokamatwa ni Heroin kilogramu 1,314.28, Cocaine kilogramu 3.04, na methamphetamine kilogramu 2,410.82.
Nyingine ni bangi kilogramu 1,758,453.58, mirungi kilogramu 202,737.51, Skanka kilogramu 423.54 na dawa tiba zenye asili ya kulevya gramu 1,956.9 na mililita 61,672.