Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Rufiji
Jeshi la Wananchi wa Tanzania limetoa magari kumi kwa ajili ya kusaidia kusafirisha vyakula kwenda kwenye makambi ya waathirika wa mafuriko walioko kwenye Wilaya za Rufiji na Kibiti Mkoa wa Pwani.
Akipokea magari hayo April 18, 2024 wilayani Rufiji, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amempongeza Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Majeshi kwa magari hayo.
Ameeleza kuwa wamepata misaada ya vyakula lakini kulikuwa na changamoto ya usafiri na Barabara katika kufikia walengwa.
Amesema magari hayo yatasaidia kufika kirahisi maeneo hayo yenye changamoto.
Vilevile Kunenge amepongeza Jeshi kwa kuendelea kulinda mipaka ya nchi na Amani kuendelea kuhudumia Jamii.
Kadhalika Kunenge,amekabidhi magari hayo kwa Wakuu wa Wilaya za Kibiti na Rufiji.