Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Pwani
Watu wawili wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili kugongana Machi 29 ,asubuhi huko Vigwaza Mizani, Wilaya ya kipolisi Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Pius Lutumo, amethibitisha kuwa,basi dogo la abiria lenye namba za usajiri T125 EAP aina ya Toyota kosta likitokea Mbeya kwenda Dar es salaam likiwa na mashabiki wa timu ya Simba liligongana na lori la mizigo aina ya Scania lenye namba za usajiri T925 BXL lenye tela namba T372 DXH lililokuwa linatokea Dar es salaam kuelekea Morogoro.
Ametaja marehemu katika ajali hiyo kuwa ni Oleison Mwakasila, anaekadiriwa kuwa na miaka 42-45, mkazi wa Kiwila mkoani Mbeya na Dereva wa gari hilo dogo aina ya kosta aitwaye Moses Mwaisela, mwenye umri kati ya miaka40-43, mkazi wa Uyole.
Lutumo ameeleza majeruhi ni Debora Barton Kajala, miaka 30, mkulima, mkazi wa Tukuyu, Devotha Emmanuel, Mwantobe, miaka 37, mkazi wa Tukuyu na Elasto David Mwalisatile, miaka 41, mkulima, mkazi wa Tukuyu Mbeya.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Msoga Halmashauri ya Chalinze na majeruhi walipelekwa katika Hospitali hiyo kwa matibabu.
Lutumo amesema chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea na mpango kazi wa muda mrefu wa kudhibiti ajali za barabarani kwa kuendelea kutoa elimu kwa madereva wa malori na mabasi lakini pia kuweka point za askari wa doria sambamba na magari ya doria barabara kuu.
Lutumo ametoa rai kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuchukua tahadhali na kuwa na udereva wa kujihami muda wote ili kuzuia ajali zinazoweza