Na Byarugaba Innocent, JamhuriMedia, Kibaha
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mheshiniwa Mussa Ndomba amefungua Kikaokazi cha siku moja kilichowakutanisha Watendaji Kata,Mitaa,Wataalam wa Kilimo,Mifugo na Maafisa Maendeleo ya Jamii kilichofanyika jana Machi 28,2024 kwenye ukumbi wa Halmashauri kikiangazia utoaji wa huduma Blbora kwa wananchi pamoja na ukusanyaji wa Mapato
Kikaokazi hiki kimehudhuliwa pia na Mkurugenzi wa Kibaha Mji Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa,Wakuu wa Divisheni na Vitengo waliotoa mada mbalimbali ikiwa ni utaratibu wa Kawaida wa kujengeana uwezo na kupeana maarifa Mapya ya kuwahudumia Wananchi.
Mheshimiwa Ndomba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa fedha kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha ili zitumike kuwaletea Maendeleo wananchi hivyo ametoa rai kwa watalaam hao kuzisimamia kikamilifu,kutunza Mazingira pamoja na kukusanya Mapato kwenye Vyanzo vilivyoanishwa kwenye mpango wa bajeti.
“Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ametuletea Mkurugenzi mpya Dkt.Rogers.Leo ametimiza siku kumi tu tangua aanze kazi hapa,lakini mambo aliyoyafanya tayari utafikiri amekuwepo kwa Mwaka mzima.Mitaro imezibuliwa,Mapato yameongezeka, watumishi wanawahi Kazini, tumpe ushirikiano”amesema Ndomba.
Akiwasilisha mada ya Ukusanyaji Mapato,Mkuu wa Kitengo cha fedha Nicholaus Haraba amesema mwongozo wa ukusanyaji Mapato wa Serikali za Mitaa unaelekeza Majukumu manne Mathalani;kusimamia ukusanyaji Mapato kwenye Kata na Mitaa,Kutunza kumbukumbu na takwimu za walipa ushuru na Kodi kwenye Kata na Mitaa,Kutambua na kutoa taarifa juu Vyanzo vipya vya mapato vilivyoibuliwa sambamba na Utoaji wa taarifa za ukusanyaji wa Mapato kwenye Kata na Mitaa;hivyo ametoa rai kwa watalaam hao kutekeleza wajibu wao kwani Serikali haiwezi kufikia malengo ya kuwapelekea wananchi Maendeleo ikiwa rasilimali fedha hazikusanywi.
Aidha,Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Leah Lwanji amesema Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa anapaswa kutekeleza Majukumu yake ikiwa ni pamoja na Kusajili na kuratibu Vikundi vya Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu,Kupokea na Kusajili maombi ya Mikopo kutoka kwenye Vikundi,Kusimamia uendeshaji na Uhai wa Vikundi pamoja na kufuatilia marejesho,kuhakikisha mikopo inayotolewa inatumika kama ilivyokusudiwa,kuratibu Mafunzo ya Vikundi pamoja na kuandaa taarifa ya mikopo iliyotolewa na kuwasilisha kwa Kamati ya huduma za Mikopo
Lwanji ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Maafisa Maendeleo ya Jamii kuongeza Kasi ya kutoa Elimu kwenye Vikundi hivyo ili wakusanye deni la marejesho kiasi cha Tsh.Bilioni 1.4 zinazodaiwa kwenye Vikundi 510 vya Halmashauri ya Mji Kibaha.
Akizungumzia vibali vya ujenzi Mhandisi Brighton Kisheo amesema ujenzi wa wowote katika mamlaka za Serikali za Mitaa ni lazima upate kibali cha ujenzi kama inavyoelekezwa kwenye vifungu Na.124 na 125 vya Kanuni ya Serikali za Mitaa za Mwaka 2008 pamoja na mwongozo uliotolewa Mwaka 2018 wa utoaji Vibali.
Mhandisi Kisheo amewataka watendaji hao kutoa Elimu ya vibali vya ujenzi kwa wananchi ili wasijenge Makazi yao holela kwani ukijenga kwa kupata kibali cha ujenzi,pamoja na mambo mengine unapanga Mji Kisasa wenye miundombinu husika.
Ametoa rai kwa wananchi kuwa vibali vya ujenzi kwani vinatolewa ndani ya wiki 1-2 na gharama zake ni nafuu.
Kwa upande wake Ally Hatibu,Mkuu wa Kitengo cha usafishaji na taka ngumu amewataka watendaji wa Kata kutoa zabuni za uondoshaji wa taka ngumu na laini kwa wakandarasi wenye uwezo kifedha na vitendea kazi imara vinavyomudu Mazingira yao ili kuondoa taka majumbani na viwandani kuzipeleka Dampo.
Wakili Salum Papen ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha huduma za Sheria ametoa wito kwa wananchi kufuata na kutii sheria bila shuruti na kwamba yeyote atakayekaidi atapelekwa mbele ya vyombo vya dola
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa amewakumbusha watumishi kutekeleza Majukumu kwa kufuata sheria,Kanuni na taratibu za nchi kwani Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imewaamini na kuwachagua kwenda kuwatumikia wananchi hivyo wamtangulize Mwenyezi Mungu katika na uaminifu na uadilifu uwaongoze.