Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Chemba ya Biashara ,Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) imefanya ziara katika mikoa 14 na kubaini changamoto nane za wafanyabishara,wenye viwanda na wakulima na kushauri mamlaka husika kupita katika maeneno hayo na kufanya maboresho.
Ziara hiyo imefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani , Lindi, Mtwara, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora , Shinyaga, Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Mara huku wakitarajia kuendelea katika mikoa mingine 12.
Akingumza na waandishi wa habari wakati akitoa thamini ya ziara hiyo Rais wa TCCIA ,Vicent Minja amesema changamoto hizo ni kufungiwa akaunti na mamlaka ya mapato (TRA), kusitishiwa huduma za mashine za kutoa risiti za kielektroniki (EFD, mazingira ya ucheleweshwaji wa huduma za biashara.
Amesema kwa upande wa madini tozo nyingi, mirahaba, TRA, service levy pia wakati huohuo kuna tozo ya Crusher, plant na elution colum, hizi zote zimeonekana kuwa changamoto kwa wafanyabiashara.
Amesema walilalamika kuwa ulipaji wa Service levy ambayo ni kuanzia 0.1 hadi 0.3%,iko juu huku huduma kama ulinzi na usafi wakigharamia wao.
“Mfumo wa stakabadhi ghalani umekuwa na changamoto, kwa mazao ya korosho, choroko na mengineyo, minada ya korosho, malipo ya vat kwa invoice ambazo mfanyabiashara hajalipwa, wazabuni kutokulipwa kwa wakati.
Amesema kingine ni Mbegu kutokuwa na ubora kunachangia uzalishaji duni wa mafuta ambao husababisha uingizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi, ambao una haribu soko la ndani, huku ufinyu wa elimu ya kilimo cha tija kwa wakulima wa alizeti wa Tanzania ukisababisha kiwanda cha alizeti na vinginevyo katika eneo la Singida, takriban asilimia 99 kusitisha uzalishaji kwa miezi sita sasa.
“Miundombinu mibovu kwenye maeneo ya biashara mfano, soko la kimataifa la vitunguu Singida,wigi wa tozo kwenye mageti.
Aidha kupitia ziara hiyo Minja amesema walifanikiwa kufanya vikao na viongozi wa serikali hasa wakuu wa mikoa,makatibu tawala ,wafanyabishara ,ofisi za chemba za mikoa na baadhi ya wilaya ili kujionea hali halisi.