RAIS Samia Suluhu Hassan amemuahidi ushirikiano wa karibu Rais mteule wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye katika kuimarisha uhusiano na tija kwa pande zote za jamhuri.
Kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Rais Samia, ameandika, matarajio yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Senegal.
“Nawasilisha pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Bassirou Diomaye Faye, Rais Mteule wa Jamhuri ya Senegal, kwa ushindi wako katika uchaguzi wa urais wa 2024 wa Senegal; na watu wa Senegal kwa uchaguzi wa amani,” ameandika Amiri Jeshi Mkuu.
Bassirou Diomaye Faye amekuwa rais mwenye umri mdogo zaidi wa Senegal, miaka 44. Amezaliwa Machi 25, 1980, katika jimbo la Thiès nchini Senegal.