Timu za soka Afrika Kusini na Cape Verde zimepangwa kukwaana katika mechi ya ufunguzi wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN), Januari 19, mwaka huu, nchini Afrika Kusini.

Ratiba iliyotangazwa katika sherehe zilizohudhuriwa pia na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, zinaonyesha kuwa wenyeji Afrika Kusini wako katika kundi A linalozijumuisha Cape Verde, Angola na Morocco.


Kundi B linaundwa na nchi za Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Niger na Mali. Mabingwa watetezi wa kombe hilo Zambia, Nigeria, Ethiopia na Burkina Faso wako katika kundi C. Timu za mataifa ya Ivory Coast, Togo, Algeria na Tunisia zinaunda kundi D.