Na Isri Mohamed
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Dkt. Damas Ndumbaro leo ameongoza zoezi la utiaji saini na mkandarasi unaohusiana na ujenzi wa uwanja mpya wa michezo Jijini Arusha.
Waziri Ndumbaro amesema kwa sasa unajengwa uwanja wa kisasa wenye thamani ya Bilioni 286, na utakuwa na uwezo wa kuchukua Mashabiki 30,000.
Makubaliano ya serikali na mkandarasi ni Uwanja huo ukamilike mwaka 2025 ili utumike mwaka 2027 kwenye michuano ya AFCON.
Dkt. Ndumbaro amesema wao kama Wizara wamependekeza uwanja huo ambao utakuwa na michezo mingine pia kama riadha, uitwe jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan Stadium kwa heshima ya Rais wa Tanzania.