Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameshinda uchaguzi wa rais kwa asilimia 87.97 ya kura, kulingana na matokeo rasmi ya kwanza yaliyooneshwa Jumapili baada ya zoezi la kupiga kura kufungwa.
Putin,71, aliyeingia madarakani mwaka 1999, alipata muhula mpya wa miaka sita kama rais, akimpita Josef Stalin kama kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi nchini Urusi.
Nikolai Kharitonov alimaliza wa pili akiwa na asilimia 4 tu, Vladislav Davankov wa tatu, na Leonid Slutsky wa nne.
Putin, katika hotuba ya ushindi mjini Moscow, aliwaambia wafuasi wake kwamba atayapa kipaumbele majukumu ya kutatua yanayohusiana na kile alichokiita “operesheni maalum ya kijeshi” ya Urusi nchini Ukraine na ataimarisha jeshi la Urusi.
“Tuna kazi nyingi mbeleni. Lakini tunapoimarishwa bila kujali ni nani anataka kututisha, kutukandamiza hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa katika historia, hawajafanikiwa sasa, na hawatafanikiwa kamwe katika siku zijazo,” amesema.